Ufunuo wa Yohana 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 2 (Swahili) Revelation 2 (English)

Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Ufunuo wa Yohana 2:1

To the angel of the assembly in Ephesus write: "He who holds the seven stars in his right hand, he who walks among the seven golden lampstands says these things:

Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; Ufunuo wa Yohana 2:2

"I know your works, and your toil and perseverance, and that you can't tolerate evil men, and have tested those who call themselves apostles, and they are not, and found them false.

tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Ufunuo wa Yohana 2:3

You have perseverance and have endured for my name's sake, and have{TR adds "have labored and"} not grown weary.

Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Ufunuo wa Yohana 2:4

But I have this against you, that you left your first love.

Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Ufunuo wa Yohana 2:5

Remember therefore from where you have fallen, and repent and do the first works; or else I am coming to you swiftly, and will move your lampstand out of its place, unless you repent.

Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Ufunuo wa Yohana 2:6

But this you have, that you hate the works of the Nicolaitans, which I also hate.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. Ufunuo wa Yohana 2:7

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies. To him who overcomes I will give to eat of the tree of life, which is in the Paradise of my God.

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. Ufunuo wa Yohana 2:8

"To the angel of the assembly in Smyrna write: "The first and the last, who was dead, and has come to life says these things:

Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Ufunuo wa Yohana 2:9

"I know your works, oppression, and your poverty (but you are rich), and the blasphemy of those who say they are Jews, and they are not, but are a synagogue of Satan.

Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. Ufunuo wa Yohana 2:10

Don't be afraid of the things which you are about to suffer. Behold, the devil is about to throw some of you into prison, that you may be tested; and you will have oppression for ten days. Be faithful to death, and I will give you the crown of life.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. Ufunuo wa Yohana 2:11

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies. He who overcomes won't be harmed by the second death.

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Ufunuo wa Yohana 2:12

"To the angel of the assembly in Pergamum write: "He who has the sharp two-edged sword says these things:

Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. Ufunuo wa Yohana 2:13

"I know your works and where you dwell, where Satan's throne is. You hold firmly to my name, and didn't deny my faith in the days of Antipas my witness, my faithful one, who was killed among you, where Satan dwells.

Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Ufunuo wa Yohana 2:14

But I have a few things against you, because you have there some who hold the teaching of Balaam, who taught Balak to throw a stumbling block before the children of Israel, to eat things sacrificed to idols, and to commit sexual immorality.

Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. Ufunuo wa Yohana 2:15

So you also have some who hold to the teaching of the Nicolaitans likewise{TR reads "which I hate" instead of "likewise"}.

Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. Ufunuo wa Yohana 2:16

Repent therefore, or else I am coming to you quickly, and I will make war against them with the sword of my mouth.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. Ufunuo wa Yohana 2:17

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies. To him who overcomes, to him I will give of the hidden manna,{Manna is supernatural food, named after the Hebrew for "What is it?". See Exodus 11:7-9.} and I will give him a white stone, and on the stone a new name written, which no one knows but he who receives it.

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Ufunuo wa Yohana 2:18

"To the angel of the assembly in Thyatira write: "The Son of God, who has his eyes like a flame of fire, and his feet are like burnished brass, says these things:

Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. Ufunuo wa Yohana 2:19

I know your works, your love, faith, service, patient endurance, and that your last works are more than the first.

Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Ufunuo wa Yohana 2:20

But I have this against you, that you tolerate your{TR, NU read "that" instead of "your"} woman, Jezebel, who calls herself a prophetess. She teaches and seduces my servants to commit sexual immorality, and to eat things sacrificed to idols.

Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Ufunuo wa Yohana 2:21

I gave her time to repent, but she refuses to repent of her sexual immorality.

Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; Ufunuo wa Yohana 2:22

Behold, I will throw her into a bed, and those who commit adultery with her into great oppression, unless they repent of her works.

nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. Ufunuo wa Yohana 2:23

I will kill her children with Death, and all the assemblies will know that I am he who searches the minds and hearts. I will give to each one of you according to your deeds.

Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. Ufunuo wa Yohana 2:24

But to you I say, to the rest who are in Thyatira, as many as don't have this teaching, who don't know what some call 'the deep things of Satan,' to you I say, I am not putting any other burden on you.

Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. Ufunuo wa Yohana 2:25

Nevertheless, hold firmly that which you have, until I come.

Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, Ufunuo wa Yohana 2:26

He who overcomes, and he who keeps my works to the end, to him I will give authority over the nations.

naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. Ufunuo wa Yohana 2:27

He will rule them with a rod of iron, shattering them like clay pots; as I also have received of my Father:

Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. Ufunuo wa Yohana 2:28

and I will give him the morning star.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Ufunuo wa Yohana 2:29

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies.